Furahia ndani ya Kila Siku

Furahia ndani ya Kila Siku

Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana, tutashangilia na kuifurahia. —ZABURI 118:24

Mojawapo ya matamanio yangu makuu katika huduma ni kuona watu wakifurahia kabisa ubora wa maisha ambayo Yesu alikufa kutupatia—sio tu kusoma kuyahusu au kuzungumza kuyahusu, lakini kutembea ndani yake na kuyazoea kama ukweli wa kila siku. Watu wengi, mimi nikiwemo, tuna mwelekeo wa kuwa na malengo kabisa. Tunadhamiria kuona ya kesho kiasi cha kwamba huwa tunakosa kuthamini na kufurahia leo kwa sababu tunawaza yajayo, tukitazamia tukio linalofuatia, tukifanya kazi kukamilisha kazi inayofuatia, na kuona kile tunachoweza kufanya katika orodha yetu ya mambo ya kufanya.

Jamii yetu ya pupa na mshinikizo inatuhimiza kutimiza kwa wingi inavyowezekana na haraka inavyowezekana—ili tuweze kutimiza hata zaidi. Kwa muda wa miaka mingi, nimejifunza kuwa, jitihada za nguvu za kukimbizana na lengo moja baada ya jingine inaweza kutufanya tukose baadhi za burudani ambazo maisha hutupatia. Mungu huwa na makusudi na mipango ambayo anataka tutimize katika nyakati zote za maisha ya humu ulimwenguni, lakini pia anataka tufurahie na kutumia vizuri kila siku tunayoishi. Mungu hunikumbusha kuishi wakati uliopo kila mara!

Kadri unavyomkaribia Mungu, ndivyo unavyogundua ni sawa kwenda polepole na kufurahia maisha yako ndani yake. Matamanio ya Mungu ni wewe kuishi katika upendo wake, amani yake, na furaha yake kila siku.


Leo ni siku amabyo Mungu amekupa; chagua kufurahia tena na kuwa na furaha ndani yake.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon