Haki ndani ya Yesu

Haki ndani ya Yesu

Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu. ISAYA 61:10

Kipaji kikubwa ambacho tutawahi kushukuru kwacho ni haki yetu ndani ya Yesu. Kupitia kwa imani ndani ya Kristo, Mungu ametuhesabia haki. Na kwa imani, ametufunika vazi la haki. Kwa maneno mengine, kwa sababu tunaamini katika haki ya Yesu kutufunika, Mungu anatuona kama wasio na makosa badala ya wakosa. Haki yake inakuwa ngao ambayo inatukinga kutokana na Shetani.

Ndani yetu na peke yetu, sisi si kitu; haki yetu ni kama nguo iliyotiwa unajisi, maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (tazama Isaya 64:6; Warumi 3:23). Lakini tumefanywa wenye haki na kupewa uhusiano mzuri na Mungu kupitia kwa imani. Kujua sisi ni wenye haki kupitia kwa kazi ya Yesu huleta amani na furaha kwa maisha yetu ambayo hakuna anayeweza kuondoa.


Sala ya Maombi

Ninakushukuru leo, Baba, kwamba nina haki kwako na ninapendeza machoni mwako kwa sababu ya kazi ya Yesu. Ninashukuru kwamba ninajua nimekubaliwa, kupendwa na kukupendeza wewe.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon