Kushughulikia Mambo Ambayo Hayajasuluhishwa

Kushughulikia Mambo Ambayo Hayajasuluhishwa

Kama yamkini kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. WARUMI 12:18

Sisi wote tuna siku ambazo huwa tunatawaliwa na hisia zetu zaidi kuliko siku zingine. Hili linaweza kufanyika kwa sababu nyingi, lakini wakati mwingine tunatawaliwa na hisia kwa sababu kitu kilitukasirisha siku iliyotangulia na hatukukishughulikia.

Ninakumbuka usiku mmoja ambapo sikuweza kulala. Mwishowe, karibu saa kumi na moja asubuhi, nilimuuliza Mungu kilichokuwa kinanifanyikia. Mara tu nikakumbuka hali ambapo nilikuwa nimemwonyesha mtu ujeuri siku iliyotangulia. Badala ya kuomba msamaha na kuomba Mungu kunisamehe, niliendelea tu na shughuli zangu za kila siku. Bila shaka, tabia yangu iliudhi roho yangu. Mara tu nilipomwomba Mungu kunisamehe na nikafanya uamuzi kumwomba huyo mtu msamaha, niliweza kulala.

Unapohisi kuhuzunika kusiko kwa kawaida au kama ambaye umebeba mzigo mzito, muulize Mungu palipo makosa. Na atakapokuonyesha, shukuru kwamba una nafasi ya kurekebisha hali hiyo.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwamba unataka niishi kwa amani. Iwapo kuna mambo ambayo sijashughulikia yanayonifanya nihisi mfadhaiko au kubebeshwa mzigo, ninakuomba unionyeshe na unipe nguvu na hekima ya kuyasuluhisha. Ninakushukuru kuwa utakuwa nami katika kila hatua safarini.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon