
Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye, macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake. WAEFESO 1:17–19 BIBLIA
Badala ya kutazama vitu hasi katika maisha, Biblia inatufundisha kuona vitu vizuri ndani ya Yesu kwa “macho ya moyo.” Waefeso 1:17-19 inasema kwamba Roho wa hekima na ufunuo ni muhimu ili:
- Tuwe na ufahamu wa Mungu, au tumjue Mungu mwenyewe. Huu sio ufahamu unaopatikana kupitia kwa elimu, isipokuwa ufunuo.
- Tujue tumaini la mwito wetu, mpango wa milele wa Mungu na vile tunavyotoshea ndani yake. Tunaweza kushukuru kwamba Mungu ametuita kuwa wanawe na kwa hivyo tunao urithi.
- Tujue kwamba tunaweza kupata ufahamu wa ufunuo wa nguvu za Mungu. Tunaweza kufanya chochote ambacho Mungu anataka tufanye kwa sababu ya ukuu wa nguvu zake.
Toa shukrani leo kwamba unaweza kumjua Mungu, kuwa na tumaini, na kuishi katika nguvu zake!
Sala ya Shukrani
Ninakushukuru Baba, kwamba umenipa amani ndani ya Yesu Kristo. Leo, nitatazama vitu vizuri katika maisha yangu na kusikiza sauti yako. Asante kwa kuwa unaniongoza na kunielekeza katika hekima na ufunuo wa Neno lako na Roho Mtakatifu wako.