Huru Kupuruka

Huru Kupuruka

Roho ya Bwana Mungu i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. —ISAYA 61:1

Upendo huwapa watu mizizi na mabawa. Hutoa hisia za umiliki (mizizi) na hisia za uhuru (mabawa). Upendo haujaribu kudhibiti au kutawala wengine kwa hila.

Yesu alisema kwamba alitumwa na Mungu kutangaza uhuru. Kama waaminio, hivyo ndivyo tunakusudiwa kufanya pia—kuweka watu huru ili watimize mapenzi ya Mungu juu ya maisha yao, sio kuwaleta chini ya udhibiti wetu.

Ushawahi kuona wazazi wakiwasukuma watoto kufanya mambo wasiotaka hata kufanya ili kutimiza dhiki ya matamanio ya wazazi wao? Ushawahi kuona mtu ambaye humgandama na kumkaba kihisia rafiki mpya, kwa sababu ana hofu ya kumpoteza mtu huyo? Hii mifano miwili inafunga badala ya kuweka huru.

Hivyo sivyo upendo wa kweli unavyofanya kazi. Upendo haujaribu kupata ridhaa ya kibinafsi dhidi ya wengine. Upendo wakati wote hutangaza ushindi. Tunapompenda Mungu na tunapowapenda wengine, tutawaruhusu kwa furaha, watu walio katika maisha yetu kufuata mpango wa Mungu kwa furaha—sio mpango wetu— na kuona wanachoweza kuwa na wanachoweza kutimiza ndani ya Yesu Kristo.


Ndege aliyetegwa hawezi kupuruka! Tangaza ushindi. Weka watu huru na uone wanayoweza kufanya.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon