Sasa, basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. WARUMI 8:1
Hatujajengwa kwa ajili ya hukumu. Mungu hakudhamiria watoto wake kushushwa chini na hukumu kwa hivyo nafsi zetu haziwezi kupambana nayo vizuri. Mungu angetaka tuhisi kuhumika, asingemtuma Yesu kutukomboa kutokana na hukumu. Aliweka juu yake, au kulipia dhambi zetu na hukumu zinazosababisha (tazama Isaya 53:6 na 1 Petro 2:24–25).
Kama waaminiyo ndani ya Yesu Kristo na wana wa kiume na kike wa Mungu, tunaweza kushukuru kuwa ametuweka huru kutokana na nguvu za dhambi (tazama Warumi 6:6–10). Hiyo haimaanishi kuwa hatutawahi kutenda dhambi, lakini inamaanisha kwamba, tukikosea, tunaweza kuungama na kupokea msamaha, na kuwa huru kutokana na hukumu. Safari yetu na Mungu kuelekea kwenye maadili mema na utakatifu ni endelevu, na wakati ule tutakapoacha kubeba hukumu ya makosa ya zamani, ndipo tutapiga hatua na kupata uhuru na furaha.
Sala ya Shukrani
Baba, ninakushukuru kwamba sihitaji kubeba hukumu na aibu ninapoishi maisha yangu. Nisaidie kusahau makosa yangu ya zamani na kutembea katika uhuru wa neema na msamaha wako.