Iweke hekalu ya Mungu katika hali nzuri

Iweke hekalu ya Mungu katika hali nzuri

Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;  1 Wakorintho 6:19

Hadi nilipofika miaka sitini na nne, sikuwa kamwe nafanya mazoezi kila wakati au kuichukua kwa uzito. Nilikuwa nikitembea na kufanya mambo machache ili kubaki na umbo mzuri, lakini sikuwa najitolea kwa zoezi. Nilikuwa nimefikia mfuko wangu wa vijisababu mara nyingi na kuja na aina zote za “sababu” mbona siwezi kufanya mazoezi.

Lakini Bwana alizungumza na moyo wangu, akanihimiza kuanza mpango mkubwa wa kufanya mazoezi ili nipate kuwa na nguvu kwa theluthi ya mwisho ya safari yangu katika maisha.

Nilikuwa na tabia nzuri ya kula, na wakati nilipomtii Bwana na kuanza kwenda kwenye mazoezi mara kadhaa kwa wiki, niliingia katika msimu mpya wa maisha. Nilionekana vizuri, nilihisi vizuri, na muhimu zaidi, nilikuwa nikimheshimu Mungu kwa kutunza mwili ambao alinipa.

Ikiwa una nafasi ya kuboresha katika eneo hili, omba na umuulize Mungu unachopaswa kufanya ili kuanza kuishi maisha bora. Neno linasema kwamba miili yetu ni hekalu ya Mungu. Na nataka kuhakikisha kwamba Mungu anapenda hekalu lake! Leo, fanya uchaguzi wa kuweka hekalu lako kwa umbo bora kwa Mungu.

OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, nataka kujitolea zaidi kwa nia ya maisha ya afya nzuri ya kimwili. Nisaidie kufanya uchaguzi mzuri ambao utaendelea kuboresha afya yangu. Mwili wangu ni hekalu lako, na nataka kuiweka kwa umbo bora kwako!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon