Je, Umesikitika na Mungu?

Je, Umesikitika na Mungu?

Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. ISAYA 55:9

Pengine unahisi kwamba Mungu alikusikitisha wakati mmoja katika maisha yako, au kwamba mojawapo ya ahadi zake kwako haikutimia. Iwapo ndivyo, ninakusihi kutambua kuwa Mungu huwa hafanyi kazi ndani ya kipimo chetu cha muda au katika njia tutakazochagua, lakini ukiendelea kumwamini, utaona wema wa Mungu katika maisha yako.

Iwapo utamwamini Mungu kila siku, shukuru kwa vitu alivyokufanyia hapo nyuma, na uamue kwamba hutawahi kukata tamaa, utamwona akifanya vitu vya ajabu katika maisha yako. Uaminifu wa Mungu humzunguka. Ni sehemu mojawapo ya tabia zake, na tunaweza kutegemea kwamba atakuwa nasi na kufanya yote aliyoahidi kufanya. Usiache masikitiko yaliyopita kukurudisha nyuma—jaribu kumwamini Mungu tena leo.


Sala ya Shukrani

Baba, nisaidie kutenga kando uchungu na masikitiko yangu na kujifunza kukuamini tena. Nimetambua kuwa hata kama sielewi mpango wako, bado ndio mzuri zaidi. Asante kwa uaminifu wako na upendo wako juu yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon