Akajibu, akawaambia, “wapeni ninyi chakula.” MARKO 6:37 BIBLIA
Wakati mmoja nilikuwa nikimwomba Mungu amsaidie rafiki aliyekuwa anapitia wakati mgumu. Alihitaji kitu, kwa hivyo nikamwomba Mungu ampe. Kwa mshangao wangu, jibu lake lilikuwa, “Acha kuniomba nitimize hitaji hilo; niombe nikuonyeshe unachoweza kufanya.” Mungu anataka tuwe tayari kuhusika. Ametubariki na vipaji, vipawa, na uwezo. Hatuhitaji tu kushukuru kwa ajili ya vitu hivyo bali tunahitajiwa kuvitumia kuwabariki wengine.
Unapopitia siku yako, ninakuhimiza kuomba na kutafuta nafasi za kufanya kile unachoamini kwamba Yesu angefanya iwapo angekuwa bado yuko duniani katika mwili. Iwapo wewe ni Mkristo, Yesu anaishi ndani yako sasa na wewe ni mjumbe wake. Hakikisha unamwakilisha vizuri. Shukuru kwa sababu ya baraka zako na utafute njia za kuwa baraka kwa wengine walio karibu nawe.
Sala ya Shukrani
Baba, nisaidie kuona mahitaji ya wale walio karibu nami. Asante kwamba umenibariki kwa njia nyingi sana. Leo ninaomba kwamba unionyeshe vile nitakavyotumia baraka hizo na wengine.