Kabili Ukweli

Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa , Kristo (WAEFESO 4:15)

Mimi na wewe tunaishi katika ulimwengu uliojaa watu wanaoishi maisha ya udanganyifu, waliovaa barakoa ya uongo, na kuficha vitu ambavyo hawataki wengine kujua. Hayo ni makosa. Lakini mambo hayo yanafanyika kwa sababu watu hawajafunzwa kutembea katika ukweli. Kama waaminiyo, tuna Roho Mtakatifu anaishi ndani yetu; Yeye ni Roho wa Kweli, na huzungumza ukweli nasi.

Wakati mwingine Shetani hutudanganya, lakini wakati mwingine tunajidanganya sisi wenyewe. Kwa maneno mengine, tunazua maisha yanayotustarehesha  badala ya kukabiliana na maisha jinsi yalivyo na kushughulikia mambo kwa usaidizi wa Roho Mtakatifu.

Roho Mtakatifu hunizungumzia na kukabili mambo katika maisha yangu kila mara, na amenifundisha kukabili mambo sio kuwa mwoga. Waoga hujificha kutokana na ukweli; wanauogopa. Usiogope ukweli. Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba Roho Mtakatifu atawaongoza katika ukweli, lakini aliwaambia kwamba hawakuwa tayari kusikia vitu fulani (soma Yohana 16:12), kwa hivyo hakuwafunulia vitu hivyo wakati huo. Roho Mtakatifu atakuzungumzia ukweli kila mara, lakini hatakuambia ukweli fulani hadi ajue kwamba uko tayari kuusikia.

Iwapo una ujasiri wa kutosha kumkaribisha Roho wa Kweli katika kila eneo la maisha yako na kumruhusu kukuzungumzia kuhusu mambo ya maisha, umejiandaa kwa safari isiyosahaulika ya uhuru na uwezo.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Usiwahi kuuogopa ukweli.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon