Kataa Kukata Tamaa

Kataa Kukata Tamaa

Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu siku zote wala wasikate tamaa. —LUKA 18:1

Watu wengi hurudi nyuma wanapopata magumu, lakini kwa usaidizi wa Mungu, tunaweza kuchuchumilia mbele bila kujali vile mambo yanavyoonekana kuwa magumu. Huwa si rahisi wakati wote lakini inafaa. Ushindi uko upande ule mwingine iwapo tutaendelea kuchuchumilia mbele.

Yesu alitwambia katika Yohana 16:33, “Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo mimi nimeushinda ulimwengu.” Eti tu kwa sababu tunapitia ugumu fulani, hatuna lazima ya kukosa tumaini na kukata tamaa. Tunaweza kuamini kwamba Yesu ameshindi kila dhiki, na tunaweza “kujipa moyo.” Hatukuumbwa kusalimu amri machoni pa dhiki; tuliumbwa tuwe na nguvu katika Bwana na katika nguvu zake kuu. Tusingekuwa na changamoto tusingehitaji imani.

Kuna mifano mingi ya watu katika Biblia ambao walikataa tu kukata tamaa. Zakayo hangezuiwa kukutana na Yesu, hata kama alikuwa na udhaifu wake. Mwanamke aliyekuwa na tatizo la damu alichuchumilia katikati ya umati na akatuzwa kwa ukakamavu wake. Walifikia malengo yao kwa sababu walichuchumilia mbele kwa ujasiri kupokea yote ambayo Mungu alikuwa nayo kwa ajili yao.

Unapokabiliwa na kizuizi, badala ya kurudi nyuma kwa hofu, mwombe Mungu akupe nguvu na ujasiri wa kwenda mbele ndani yake.


Unapohisi kuondoka, kiri kwamba: “Sitakata tamaa! Mungu yuko nami, na atanisaidia kusonga mbele hatua baada ya hatua kwa wakati wake!”

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon