Kipaji cha Bure cha Upendo wa Mungu

Kipaji cha Bure cha Upendo wa Mungu

Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. WAEFESO 1:5

Kuna kitu kimoja tu unachoweza kufanya na kipaji cha bure, na hicho ni kipokee na ushukuru. Ninasihi kuchukua hatua ya imani sasa hivi na kusema kwa sauti, “Mungu ananipenda bila masharti, na ninapokea upendo wake!” Huenda ukahitaji kusema hivyo mara mia moja kwa siku kabla izame, lakini ikifanya hivyo, itakuwa ni siku ya furaha sana katika maisha yako.

Kujua kwamba unapendwa na mtu ndicho kitu kizuri sana na chenye hisia ya kufariji sana ulimwenguni. Mungu hakupendi tu bali pia anakupa watu wengine ambao watakupenda kwa kweli. Anapowaleta, hakikisha unashukuru kwa ajili ya watu hao wakati wote. Kuwa na watu ambao kwa kweli wanakupenda ni mojawapo ya vipaji vyenye thamani ulimwenguni.

Tenga wakati kumshukuru Mungu kwa upendo wake na kwa ajili ya watu wanaokupenda! Ni kipaji chake kwako na, ninaamini mojawapo ya vipaji vyenye thamani ambavyo utawahi kupokea.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa kipaji cha bure cha upendo wako. Ninashukuru kwamba unanipenda bila masharti na umetia watu wanaonipenda katika maisha yangu pia. Sitapuuzi upendo wako na, ingawa siwezi kulipa upendo wako, ninataka kuishi maisha yangu kwa ajili yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon