Kipawa cha Haki

Kipawa cha Haki

. . . Bali na kwa ajili yetu sisi mtakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu. —WARUMI 4:24

Mmojawapo wa ufunuo wa kwanza ambao Mungu alinipa katika Neno ulikuwa kuhusu haki. Kwa “ufunuo,” ninamaanisha kitu unachoelewa kufikia mahali ambapo kinakuwa sehemu yako. Maarifa hayo hayako tu mawazoni mwako, bali katika moyo wako. Unahakikishiwa ukweli.

Haki ni kipawa cha Mungu kwetu sisi. “kinahesabiwa na kupewa” sisi kutokana na kuamini kwetu kile ambacho Mungu alitufanyia kupitia kwa Mwanawe, Yesu Kristo. Yesu, asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye (2 Wakorintho 5:21).

Zaidi ya yote, shetani hataki tutembee katika ukweli kwamba tuko katika haki ya Mungu. Anataka tuhisi hatuna usalama, tuaibike, tuhukumike na tujilaumu ili tuondoke kwa Mungu badala ya kufurahia kuwa karibu naye.

Yesu anataka tujue kwamba tuna haki kwa Mungu kwa sababu ya kile ambacho ametutendea. Anataka tumfurahie na kufurahia kuishi katika uhusiano naye. Pokea kipawa cha msamaha wa Mungu, rehema na haki leo na uanze safari ya uhuru na furaha.


Unaweza kuwa na ufunuo wa kipawa cha haki kwa kutafakari Neno la Mungu na kuamini linachosema kukuhusu ndani ya Yesu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon