Kuamini Wewe Hudhibiti Nafsi Yako

Kuamini Wewe Hudhibiti Nafsi Yako

Bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki na mtakatifu na mwenye kudhibiti nafsi yake. TITO 1:8 BIBLIA

Mara nyingi huwa ninasikia watu wakisema, “Mimi sio tu wa kudhibiti nafsi yangu,” au “Sina tu kiasi,” na wanataja eneo fulani kama kula, kufanya mazoezi, au kupanga vitu vizuri. Iwapo wewe ni mmojawapo wa watu kama hawa ambao wanaamini kuwa hawawezi kudhibiti nafsi zao, basi ninataka kukuhimiza kubadilisha mawazo yako.

Mtume Paulo alieleza kwamba, Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo, na ya moyo wa kiasi (tazama 2 Timotheo 1:7). Shukuru—tayari Mungu amekupa kiasi unachohitaji! Ni wakati wa kuanza kugeuza nia yako upya kwa kutafakari fikra hii: nina nidhamu na kiasi.

Hutawahi kuinuka juu ya kile unachoamini, unapozidi kuamini kuwa wewe si mtu mwenye nidhamu, basi hutawahi kuwa. Badala yake, amini Neno la Mungu na uishi ndani ya ukweli wake. Una kiasi, na una nidhamu!


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwamba umenipa kila nidhamu na kiasi ninachohitaji. Nisaidie kugeuza nia yangu upya kulingana na ukweli wa Neno lako. Ninakushukuru kwamba kwa usaidizi wako, ninaweza kuishi maisha ya kushinda yenye nidhamu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon