Kubadilishana Kuzuri

Kubadilishana Kuzuri

Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye. 2 WAKORINTHO 5:21 BIBLIA

Kubadilishana kuzuri ambako hufanyika tukimpa Mungu maisha yetu ni kitu tunachoweza kushukuru kwacho wakati wote. Wokovu una maana kuwa tunampa Mungu tulicho nacho naye anatupa alicho nacho.

Anachukua dhambi zetu zote, makosa, udhaifu, upungufu, na kutupatia uwezo wake, haki na nguvu zake. Anachukua maradhi na ugonjwa wetu na kutupatia uponyaji na afya yake. Anachukua maisha yetu ya hapo nyuma yaliyovurugika, yaliyojaa kushindwa na kutupatia tumaini la mustakabali wenye nuru.

Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi (tazama Isaya 64:6). Lakini ndani ya Yesu, tuna mustakabali wa kushukuru kwao—mmoja unaostahili kutarajiwa. Neno “ndani ya Yesu” kwa wepesi linamaanisha kwamba tumeweka imani yetu kuhusu kila kipengele cha maisha yetu ndani yake. Tuko katika agano na Mungu aliye Mkuu. Fikra ya ajabu ilioje!


Sala ya Shukrani

Baba, ninapohisi kwamba sifai au kuhumika, nisaidie kukumbuka niliye katika Kristo. Asante kwamba nimesamehewa, kukubalika, mwenye haki, nguvu na uwezo kwa sababu ninapatikana ndani yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon