Kufanya kila Siku Isiwe ya Kawaida

Kufanya kila Siku Isiwe ya Kawaida

. . . Lakini Daudi akajitia nguvu katika Bwana Mungu wake. 1 SAMWELI 30:6

Hakuna siku itakayoonekana ya kawaida iwapo tutakuwa wenye shukrani kwa kila kipaji ambacho Mungu hutupatia kila siku inapoanza. Mtazamo wa mambo usio wa kawaida unaweza kubadilisha siku ya kawaida ikawa ya matukio ya kuajabisha. Yesu alisema alikuja ili tuwe na uzima na tuufurahie (tazama Yohana 10:10). Tukikataa kuyafurahia basi sio makosa ya mtu yeyote bali yetu wenyewe.

Ningependa kupendekeza kuwa uwajibikie furaha yako na usiwahi tena kumpa mtu yeyote kazi ya kukufurahisha kila wakati. Unaweza kudhibiti unachofanya, lakini huwezi kudhibiti kile watu wengine wanafanya. Kwa hivyo huenda usiwe na furaha wakati mwingi ukiwategemea kama chanzo cha furaha yako. Mwandishi wa Zaburi Daudi alisema kwamba alijitia nguvu katika Bwana, na kama anaweza kufanya hivyo, basi tunaweza kufanya hivyo pia.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwa ajili ya hii siku mpya ambayo umenipa. Bila kujali vitendo au nia za wengine, nitaifurahia siku hii kwa sababu Wewe ndiwe chanzo cha furaha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon