Kufurahia kila Hatua Njiani

Furahini katika Bwana siku zote; tena nasema furahini! —WAFILIPI 4:4

Paulo alihisi kufurahia ndani ya wema wa Bwana kulikuwa muhimu sana hata anatuambia mara mbili katika huu msitari kutoka Wafilipi kwamba tufurahi. Anatuhimiza katika mistari inayofuatia kwamba tusiwe na wasiwasi wala kuhangaika kuhusu kitu chochote lakini tuombe na kumpa Mungu shukrani kwa kila kitu—sio baada ya kila kitu kuisha.

Tukingoja hadi kila kitu kiwe kitimilifu, kabla ya kufurahia na kushukuru, hatutakuwa na furaha sana. Kujifunza kufurahia maisha hata katikati ya hali ngumu ni mojawapo ya njia za kumkaribia Mungu. Paulo anaandika kwamba “kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo toka utukufu hata utukufu, (2 Wakorintho 3:18). Hiyo ina maana kuwa tunaweza kuufurahia utukufu ambao huwa katika kila kiwango cha ustawi wetu, kwa sababu kila siku mpya ni hatua nyingine ya kuelekea kuwa yule mtu anatuunda tuwe.

Mara ya kwanza nilipoanza huduma yangu, furaha yangu ilitegemea hali yangu. Mwishowe Bwana alinionyesha mlango wa kwenda furahani. Alinipa upenyo kwa kunifundisha kwamba utimilifu wa furaha hupatikana katika “uwepo” wake—sio katika vipawa vyake (Zaburi 16:11).


Furaha ya kweli hutambuliwa tunapoutafuta uso wa Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon