Kuishi kwa Amani

Kuishi kwa Amani

Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu wala msiwe na woga. YOHANA MTAKATIFU 14:27

Amani ni mojawapo ya vitu muhimu sana katika kufurahia maisha yako.

Maisha ya mfadhaiko na kung’ang’ana, maisha bila amani, ni matokeo ya kufikiri kuhusu mambo ambayo huna uwezo juu yake. Unapokuwa na wasiwasi kuhusu vitu usivyoweza kudhibiti, msongo wa mawazo na fadhaa vinaanza kuingia katika maisha yako.

Mtume Paulo anasema, “Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.” Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.” (Wafilipi 4:6-7 Biblia).

Mara tu tunapogundua tunang’ang’ana na kitu na kuhisi mfadhaiko, tunahitaji kuanza kuomba na kumpa Mungu hali hiyo mara moja, huku ukiwa na shukrani kwamba atatoa kulingana na mapenzi Yake na kutupatia amani. Mimi na wewe hatujaitiwa maisha ya mfadhaiko na kung’ang’ana. Yesu alikuja ili tuwe na haki, furaha na amani!


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwa amani. Ni kipawa cha ajabu ambacho umenipa, na ninaomba usaidizi wako ili wakati wote niwe na amani katika kila hali.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon