Kuja kwa Ujasiri Mbele ya Mungu

Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana na nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. —WAEBRANIA 4:15–16

Yesu huelewa udhaifu wetu wa kibinadamu kwa sababu alijaribiwa kwa kila njia tunayojaribiwa, ilhali bila kutenda dhambi. Kwa hivyo, kwa kuwa Yesu ni kuhani wetu mkuu, akituombea mbele za Baba, tunaweza kuja kwa ujasiri kwenye kiti cha enzi kupokea neema.

Tayari Mungu ametoa suluhu kwa kila kosa, udhaifu na kushindwa kwa binadamu. Wokovu na msamaha usiokoma wa dhambi zetu ni vipawa tulivyopewa na Mungu kwa sababu ya kumkubali Mwanawe , Yesu Kristo. Ndani yake unaweza kupata msamaha kwa kila kitu kibaya utakachowahi kufanya.

Lakini neema ya Mungu haimaanishi hakabiliani na dhambi katika maisha yetu. Dhambi huzalisha kufungwa na mateso. Ndiyo maana Mungu anatuita tutubu dhambi zetu. Ingawa Mungu huwa hatushtumu, hutuhukumu kwa dhambi zetu. Hututia hatiani ili tutubu, tubadilishe tabia zetu na kupata uhuru ndani ya Kristo.

Kwa sababu ya Yesu, tunaweza kupokea msamaha, tukaweka kando tabia za dhambi, na kuja kwa ujasiri mbele ya kiti cha Mungu cha neema. Haya matendo yote ni vipengele muhimu vya kuishi katika uhusiano wa karibu na Mungu.


Hata tukiwa sawa kabisa, tunaweza kufanya makosa. Kuishi chini ya hukumu hakutatusaidia kuishi maisha ya utakatifu zaidi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon