
Kwa Bwana ampendaye humrudi, kama vile baba mwanawe ampendezaye. —MITHALI 3:12
Pengine umekuwa uking’ang’ana na kujikubali. Unaona maeneo ndani yako ambapo mabadiliko ni muhimu. Unatamani kuwa kama Yesu. Ilhali ni vigumu kwako kufikiria au kusema, “Ninajikubali.” Unahisi kwamba kufanya hivyo itakuwa kukubali mambo yasiyo sawa kukuhusu, lakini sio hivyo. Tunaweza kujikubali na kujikumbatia kama viumbe wa kipekee wa Mungu, na bado tukose kupenda kila kitu tunachofanya.
Mungu atatubadilisha, lakini hatuwezi kuanza utaratibu wa mabadiliko hadi hili suala la kujikubali lishughulikiwe katika maisha yetu binafsi. Tunapoamini kwa kweli kuwa Mungu anatupenda bila masharti vile tu tulivyo, basi tutakuwa na ukaribu naye, na tutakuwa tayari kupokea adhabu yake, ambayo ni muhimu kwa mabadiliko ya kweli.
Mabadiliko huhitaji adhabu—watu ambao hawajui kuwa wanpendwa huwa na wakati mgumu sana wanapopokea adhabu. Adhabu ni njia ya Mungu kutupatia mwelekeo wa kiungu kwa ajili ya maisha yetu. Anatuongoza kwa kutuelekeza kwa vitu vyema, lakini tukiwa hatuna salama, tutakuwa tunahisi kuhukumika kwa adhabu badala ya kuikumbatia kwa furaha teletele.
Mungu huwa hayakubali matendo yetu yote, lakini anatupenda na kutukubali kama wanawe wapendwa.
Kuwa mwenye subira kwako mwenyewe. Endelea kupiga hatua na kuamini kwamba unabadilika kila siku.