Kumshukuru Mungu Mchana Kutwa

Kumshukuru Mungu Mchana Kutwa

Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana! (Hallelujah!) ZABURI 150:6

Mojawapo ya vitu vizuri ambavyo tunaweza kufanya mchana kutwa ni kusifu Mungu huku tukifanya kazi. Haijalishi unachoweza kuwa unajaribu kufanya—nyumba yako, ndoa yako, biashara yako, usalama wa kifedha, mpango wa mazoezi, au uhusiano wa ndani na Mungu—usisahau kuabudu unapofanya kazi.

Kumbuka kumsifu Mungu na kumshukuru hata kwa hatua ndogo za maendeleo. Hauhitaji kutunga sifa kutokana na kusifu kwako; kuwa tu na moyo wenye shukrani unaosema, “Ninakupenda, Bwana. Ninakuabudu. Siwezi kufanya hili bila wewe. Ninahitaji usaidizi wako leo. Asante kwa kunipa lengo la kutimiza na kwa kunisaidia kulifanikisha.”


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, hata kwa hatua ndogo kabisa za maendeleo ambazo unaniwezesha kupiga katika maisha yangu. Ninakupenda na ninajua kwamba unafanya kazi nzuri ndani yangu na kupitia kwangu. Asante kwa kila kitu ambacho umefanya katika maisha yangu na kila kitu ambacho bado utafanya.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon