kushinda mawazo ya jangwa

kushinda mawazo ya jangwa

Bwana, Mungu wetu, alituambia huko Horebu, akasema, Mlivyokaa katika mlima huu vyatosha; Kumbukumbu la torati 1:6

Waisraeli walizunguka jangwani kwa miaka arobaini kufanya kile kilikuwa ni safari ya siku kumi na moja. Kwa nini?

Mara moja, nilipozingatia hali hii, Bwana aliniambia, “Waisraeli hawakuweza kuendelea kwa sababu walikuwa na mawazo ya jangwa.” Waisraeli hawakuwa na maono mazuri kwa maisha yao-hawakuwa na ndoto. Walihitaji kuyaacha mawazo hayo na kumwamini Mungu.

Hatupaswi kuona Waisraeli kuwa wa kushangaza kwa sababu wengi wetu hufanya mambo yale yale waliyofanya. Tunaendelea kuzunguka milima hiyo badala ya kufanya maendeleo, na inachukua miaka yetu kupata ushindi juu ya kitu ambacho kinaweza kushughulikiwa haraka.

Tunahitaji mawazo mapya. Tunahitaji kuanza kuamini kwamba Neno la Mungu ni kweli. Mathayo 19:26 inatuambia kwamba kwa Mungu vitu vyote vinawezekana. Yote anayohitaji ni imani yetu ndani yake. Anahitaji sisi kuamini, na Yeye atafanya mengine.

Bwana anasema jambo lile kwetu leo kama alivyowaambia wana wa Israeli: Umekaa muda mrefu juu ya mlima huu. Ni wakati wa sisi kuendelea!


OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, nimekuwa na muda wa kutosha kwenda karibu na milima mingi ya zamani katika maisha yangu. Nikiwa na wewe, najua ninaweza kuendelea, hivyo nitaweka imani yangu ndani yako na kuachana na mawazo yangu ya jangwani!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon