Kushirikiana na Mungu

Kushirikiana na Mungu

Ombeni bila kukoma. 1 Wathesalonike 5:17

Maombi ndiyo faida kubwa sana ya maisha yetu. Sio kitu ambacho lazima tufanye; ni kitu tunachopata kufanya! Maombi ni mojawapo ya njia tunazoshirikiana na Mungu ili kuona mipango na makusudio yake yakitimia katika maisha yetu na katika maisha ya wale tunaowapenda. Ni njia ambayo binadamu ulimwenguni wanaweza kuingia katika uwepo na nguvu za ajabu za Mungu.

Maombi huturuhusu kumweleza Mungu yaliyo mioyoni mwetu, kusikia anavyotuongoza, kuonyesha shukrani zetu, na kujua vile tutakavyotambua na kufurahia vitu vyote vikuu alivyo navyo kwa ajili yetu. Nimesikia ikisemwa kwamba “kushindwa kwote ni kushindwa kuomba.” Kuwasiliana na Mungu kwa kweli ni faida kubwa kabisa ninayojua, na pia ndiyo faida kubwa sana ninayojua. Usifanye maombi yatatize au kuwa magumu. Yafanye yawe rahisi na ufurahie kila dakika unayotumia na Bwana katika maombi.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwa faida kubwa ya kuja kwako kwa maombi. Ni ajabu kufikiri kwamba ninaweza kuingia katika uwepo wako kwa shukrani leo. Asante, Bwana, kwa kusikiza maombi yangu na kwa kuniongoza ninapoendelea na shughuli zangu za kila siku.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon