Kustawisha Uwezo Wako

Kustawisha Uwezo Wako

Je! Hamjui ya kuwa wale washindanao, kwa kupiga mbio hupiga mbio wote lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo ili mpate. — 1 WAKORINTHO 9:24

Tunaposonga karibu na Mungu kwa kuchagua kuacha woga na kujishuku, tunaweza kustawisha uwezo wetu na tukafanikiwa kuwa yote ambayo Mungu alikusudia tuwe. Lakini hatuwezi kustawisha uwezo wetu iwapo tunaogopa kutofanikiwa. Tutakuwa na woga mwingi wa kushindwa ua kufanya makosa kiasi kwamba itatuzuia kuchukua hatua.

Mara kwa mara huwa ninaona watu walio na uwezo mkubwa, ilhali nafasi zikitokea wanazikataa haraka. Wakati mwingi huwa hawana hakika na hukosa kujua kwamba wangetimiza mambo mengi iwapo tu wangechukua hatua kwa imani wakijua kwamba Mungu yuko pamoja nao.

Mara nyingi tukikosa kuwa na uhakika, tutakaa na kile ambacho tuna uhakika nacho na tunachokifahamu vizuri kuliko kuchukua hatua na kushindwa. Tunajiepusha na kuchukua wajibu mkubwa zaidi kwa sababu tunahisi hatuko tayari—lakini ukweli ni kwamba hakuna mmoja wetu ambaye huwa tayari. Hata hivyo Mungu huwa tayari wakati wote, na anapoanza kutenda kazi katika maisha yako, unaweza kujua kwamba atakupa vitu vyote unavyohitaji wakati ule unapovihitaji.


Kujiegemeza kiunyenyekevu kwa Mungu husababisha mafanikio. Imani yetu inapokuwa ndani ya Kristo na sio ndani yetu, tunakuwa huru kustawisha uwezo wetu, kwa sababu tunakuwa huru kutokana na hofu ya kushindwa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon