Kuwa Mzuri katika Kumwamini Mungu

Kuwa Mzuri katika Kumwamini Mungu

Bwana ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao. Nahumu 1:7 Biblia

Tunaweza kutumia muda wetu wote tukifikiri na kuongea kuhusu yaliyo mabaya uliwenguni au tunaweza kuchagua kumakinikia mambo mazuri. Tunaweza kufikiri kuhusu kilicho kibaya na mwanafamilia, rafiki, au mafanyikazi mwenzetu, au tunaweza kutafuta kimaksudi kilicho kizuri na kukipa kipaumbele.

Iwapo vitu tisa ni vibaya na tuone tu viwili ambavyo tunahisi kwamba viko sawa, tunaweza kufanya hivyo viwili vionekane vikubwa kuliko vile tisa—kisha tudhamirie kuvimakinikia. Nimesikia watu wengi wakisema, “Siwezi tu kudhibiti maisha yangu ya mawazo.” Ukweli ni kwamba walichagua kumakinikia mawazo yasiyo mazuri.

Chagua kumakinikia mawazo ya kiungu yaliyojaa imani. Acha mwitiko wako katika hali yoyote ile uwe wa kuona mema, sio mabaya. Ongea kwa sauti na useme, “Ninamwamini Mungu kabisa. Ninajua ana mpango. Atafanya kitu kizuri katika maisha yangu!”


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa kuwa kuna vitu vizuri vya kufikiria vinavyonizunguka. Nisaidie kuona mema ndani ya watu, sio mabaya. Asante kwa kuwa ninaweza kuchagua fikra zangu na ninaweza kufurahia maisha uliyonipa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon