Njia bora ya kuanza

Njia bora ya kuanza

Kutangulia mapambazuko naliomba msaada, Naliyangojea maneno yako kwa tumaini. Zaburi 119:147

 Wewe huanza aje siku yako? Je, unatoka haraka kutoka kwenye kitanda na uwe na muda usiotosha kujiandaa? Je, unageukia kwenye TV? Je, unafanya mazoezi? Chochote kile utaratibu wako wa asubuhi unaweza kuwa, swali muhimu zaidi unayohitaji kujiuliza ni, Je, Mungu anacheza nafasi ipi wakati mimi huanza siku yangu?

Nilichukua miaka mingi ili nifahamu jambo hili, lakini sasa ninajua kuwa njia bora kabisa ya kuanza siku yangu ni kwa kumshukuru Mungu kwa kile alichonifanyia na kumwuliza jinsi ninaweza kuwa baraka kwa watu wengine.

Ninakuhimiza kutumia muda kila asubuhi kuzingatia mambo mema ambayo Mungu amefanya katika maisha yako. Fikiria juu ya hatari na shida alizokupitisha, njia ambazo alikuponya na kukubadilisha, na jinsi ni vizuri kujua kwamba anakujali na kusikia maombi yako.

Unapojifunza kuweka mawazo yako juu ya Mungu asubuhi kila siku, atakupa amani na furaha yote unayohitaji kumtumikia wakati unapoendelea siku zako zote.

 OMBI LA KUANZA SIKU

 Bwana, ninafanya uamuzi leo kukufuatilia Wewe jambo la kwanza wakati ninapoamka kila asubuhi. Hakuna la muhimu zaidi kuliko kukutafuta na kupokea amani na furaha yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon