Kuwa na Furaha Unaposaidia

Kuwa na Furaha Unaposaidia

Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema. 2 WAKORINTHO 9:8 BIBLIA

Uchunguzi wa kanuni muhimu ulifanywa na Bernard Rimland, mkurugenzi wa taasisi ya Child Behavior Research. Kila mwanafunzi aliyehusika katika uchunguzi huo aliombwa kuorodhesha watu kumi ambao aliwajua vizuri ili kuwapa vibandiko vya wenye furaha au wasio na furaha. Halafu walikuwa wapitie kwa hiyo orodha tena na kuwapa vibandiko vya ubinafsi au wasio na ubinafsi. “Watu walio na furaha sana ni wale ambao huwasaidia wengine,” akahitimisha.

Mungu hutupatia uwezo na nafasi ya kusaidia wengine mchana kutwa. Tukitenga muda na kuwa baraka, inatufanya kutofikiria sana kuhusu kile tusichokuwa nacho, na kushukuru kwa kile tulicho nacho na hatimaye kufikia kiwango kipya cha furaha. Usiache siku ipite kabla hujamsaidia mtu.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba kila siku unanipa nafasi ya kuwa baraka kwa wengine. Umenibariki na vitu vingi. Ninataka kutumia kile ulichonipa kumbariki mtu mwingine leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon