Nathani akamwambia mfalme, haya fanya yote yaliyomo moyoni mwako maana Bwana yu pamoja nawe. —2 SAMWELI 7:3
Moyo unaotaka ni moyo ambao “unataka ku” Iwapo kuna kitu tunachotaka kufanya kabisa, iwavyo, huwa tunapata vile tutakavyokifanya. Kwa usaidizi wa Mungu na moyo unaotaka, tunaweza kuwa na uhusiano wa karibu naye, kudumisha usafi wa nyumba zetu, kuweka akiba ya pesa, kulipa madeni, au kufikia lengo lingine lolote tulilojiwekea maishani. Ushindi wetu au kushindwa unategemea “kutaka ku” kwetu.
Mara nyingi huwa tunamlaumu shetani kwa kushindwa kwetu, watu wengine, mambo yaliyopita, na mengine mengi. Lakini cha msingi hapa ni kwamba hatuna aina nzuri ya kutosha ya “kutaka ku.”
Ukitaka kweli kuwa karibu na Mungu, ninaamini utakuwa. Moyo wako unaotaka utakufanya umtafute kwa jitihada. Utachagua kutumia muda wako katika maombi kila siku na kusoma Neno la Mungu. Mungu atauona moyo wako na kukukaribia hata unapozidi kumkaribia.
Mara nyingi huwa hatuhisi kufanya tunachotaka kufanya, lakini si lazima ufanye uamuzi wako kwa kutegemea hisia zako.