Kuwa Na Uelekevu Wa Nia

Kuwa na Uelekevu wa Nia

Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndiyo yalivyo. —Matendo Ya Mitume 17:11

Biblia inasema kwamba tunastahili kuwa na nia elekevu. Hiyo ina maana tunaweza kuwa na nia zilizofunguka kwa mapenzi ya Mungu juu yetu, mapenzi yoyote yale kwetu.

Nilizungumza na mwanamke mdogo mmoja wakati mwingine ambaye alikuwa amewahi kuvunjika moyo kwa sababu ya uchumba uliovunjika. Alikuwa akitaka uhusiano huo uendelee na alikuwa akiwaza, kutumaini, na kuamini kwamba aliyekuwa mchumba wake atahisi vile alikuwa akihisi.

Nilimshauri kuwa na “nia elekevu” iwapo mambo hayatakuwa alivyotarajia. Akaniuliza, “Huo si uhasi?”

Hapana, si uhasi. Uhasi utasema, “maisha yangu yamefikia kikomo. Hakuna mtu mwingine atakayenitaka. Nitateseka milele.”

Kuwa na nia chanya husema, “kwa kweli nimehuzunika kwamba hili limefanyika, lakini nitamwamini Mungu. Nitaomba na kuamini uhusiano wetu utarejeshwa; lakini zaidi ya yote, ninataka mapenzi kamilifu ya Mungu. Isipokuwa ninavyotaka, nitaishi, kwa sababu Yesu anaishi ndani yangu. Huenda ikawa vigumu lakini ninaamini Bwana. Ninaamini kwamba, mwishowe, kila kitu kitakuwa kizuri.


Zoea kuwa chanya katika kila hali inayotokea. Mungu ameahidi kuleta mema kutokana na yale yanayotokea katika maisha yako wakati huu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon