Kwa Muda Gani, Bwana?

Kwa Muda Gani, Bwana?

Bali wao wamngojeao Bwana [wanaomtarajia, kumtafuta na kumtumainia] watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. —ISAYA 40:31

Kumngoja Mungu hakumaanishi kwamba tusifanye lolote, huku tukimtarajia Mungu kutufanyia kila kitu. Kwangu mimi inamaanisha kwamba, ninangoja nikitarajia Mungu kunipa mwelekeo iwapo kuna kitu anataka nifanye, huku nikendelea kuamini atafanya kile ambacho yeye peke yake anaweza kufanya. Mara nyingi nimemngoja Bwana na kuweka tumaini langu ndani yake, akanionyesha vitu ambavyo vinahitaji kurekebishwa katika tabia au fikra zangu. Unaona, Mungu hataki tu kubadilisha hali zetu, lakini anataka kutubadilisha pia.

Tunapotumia muda mtulivu kuwa na Mungu, anatufunulia vitu na tunafanywa wapya katika uwepo wake. Ukaribu na undani na Mungu ni mojawapo ya faida kuu kwetu kama watoto wa Mungu. Kadri tunavyotumia muda kuwa naye, ndivyo tunavyobadilishwa kwa mfano wake. Soma Neno la Mungu na ulipokee kama barua yako binafsi kutoka kwake hadi kwake. Itakufariji na kukurekebisha. Mngoje Mungu na moyo unaoamini na kutarajia, na utazamie vitu vyote vizuri ambavyo amepanga kwa ajili yako.


Mungu atakubadilisha kidogo kidogo kila siku, unapomwamini.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon