Kukabili Changamoto Yoyote Mpya kwa Ujasiri

Kukabili Changamoto Yoyote Mpya kwa Ujasiri

Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, wewe unanijia mimi na upanga, na fuo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. 1 Samweli 17:45 Biblia

Mara nyingi huwa tunaogopa majaribu na dhiki. Tunapoona tu ishara ya kwanza ya dhiki, tunaanza kurudi nyuma kwa woga. Waaminio walioishi katika karne zilizopita walionekana kudhihirisha nguvu tofauti kuliko wengi wanavyofanya leo. Badala yake tumezoea starehe na huwa tunatatizika tunapopata dhiki ya aina yoyote ile; hututia hofu.

Acha tukumbuke vile Daudi alilikabili jitu Goliathi na tuwe na furaha na shukrani kuwa tunaweza kuwashinda adui zetu pia. Tunaweza kushambulia hofu badala ya kuiacha itutawale. Wewe ni zaidi ya hisia zako. Wewe ni mwana wa Mungu uliye na nguvu, hekima, na unayependwa na unaweza kufanya chochote unachohitaji kufanya maishani kupitia kwa Kristo, ambaye ni nguvu zako (tazama Wafilipi 4:13).


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwa nguvu nilizo nazo kwa sababu uko nami. Licha ya changamoto kuonekana kuwa ngumu, nitaishambulia kwa ujasiri kwa sababu ninajua hakuna kisichowezekana kwako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon