Lakini, Je, Iwapo Nitamkosa Mungu?

Lakini, Je, Iwapo Nitamkosa Mungu?

Na masikio yako yatasikia neno nyuma yako likisema njia ni hii, ifuateni mgeukapo kwenda mkono wa kulia, na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto. ISAYA 30:21

Wakati mwingine tunakuwa na kusita katika maisha kwa sababu tunaogopa kwamba huenda “tunamkosa Mungu,” au kufanya kitu kibaya tunapojaribu kumfuata. Acha nikuhimize kwa kukwambia kwamba ukikosa mapenzi ya Mungu juu yako kwa namna moja au nyingine, usiwe na wasiwasi—Atakupata. Ninafikiri sisi wote hupotea maishani wakati mwingine na kuhitaji rehema ya Mungu kuonekana na kuturudisha kwenye njia sahihi. Leo, unaweza kushukuru Mungu kwamba ni mwaminifu kunyosha kila njia iliyopinda mbele yako.

Iwapo unaogopa kufanya uamuzi mbaya kuhusu mwelekeo wako katika maisha, kile unachohitaji kufanya ni kukumbuka vile Mungu anakupenda na kutazama ushuhuda wa watu ambao wamekutangulia. Biblia imejaa visa vya uongozi na upaji wa ajabu wa Mungu.

Tunapochukua hatua ya imani baada ya kuomba na kumtafuta Mungu, tukifanya kosa, Mungu ataturudisha njiani. Shukuru kwamba Mungu anaweza kufanya hilo linaloitwa kosa ligeuke kwa namna yoyote ile kwa wema wetu.


Sala ya shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwamba unaona moyo wangu. Nikikosa sauti na njia yako katika maisha yangu, ninakushukuru kwamba utanipata na kunielekeza katika njia inayofaa. Ninaamini uongozi wako na leo ninachagua kuishi bila woga wa kukukosa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon