Makao Yake

Hamjui ya kuwa nyinyi mmekuwa hekalu la Mungu na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? (1 WAKORINTHO 3:16)

Nimeshangazwa na kustaajabu ninapofikiria kuhusu baraka kuu ya Roho Mtakatifu kuishi ndani yetu. Hutuchochea kufanya mambo makuu. Hutujaza nguvu za kufanya kazi zetu zote. Hukaa katika umoja wa karibu nasi, bila kutuacha wala kutusahau.

Hebu fikiria tu- iwapo mimi na wewe ni waaminio ndani ya Yesu Kristo, sisi ni makao ya Roho Mtakatifu wa Mungu! Tunafaa kutafakari ukweli huu mara nyingi hadi uwe ufunuo wa kibinafsi katika maisha yetu. Tukifanya hivyo hatutawahi kukosa usaidizi, kukosa tumaini, au nguvu, kwa sababu anaahidi kuwa nasi, kutuzungumzia, kututia nguvu, na kutuwezesha. Hatutawahi kuwa bila rafiki au mwelekeo, kwa kuwa anaahidi kutuongoza na kuwa nasi katika kila kitu tunachofanya.

Paulo alimwandikia mfuasi wake mchanga Timotheo, “Ilinde [kwa uangalifu mkuu] amana [ukweli] nzuri kwa [kwa usaidizi wa] Roho Mtakatifu akaaye ndani yako” (2 Timotheo 1:14).

Ukweli unaojua kuhusu Roho Mtakatifu ni wa thamani sana; ninakuhimiza kuutunza na kuuweka moyoni mwako. Usiuruhusu kukukwepa. Kwa kuwa wewe ni aaminiye ndani ya Yesu, Roho Mtakatifu yuko ndani yako kukusaidia sio tu kuhifadhi ulichosoma kumhusu, lakini kukusaidia kukua na kukuwezesha kuwapa wengine. Mfurahie, mheshimu, mpende  na kumsujudu. Yeye ni mwema sana, mkarimu, na wa maajabu. Ni wa ajabu na wewe ni makao yake!

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Sema kwa sauti mara kadhaa kwa siku: “Mimi ni makao ya Mungu. Hufanya makao yake ndani yangu.”  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon