Maombi Hayahitaji Kuwa Marefu

Maombi Hayahitaji Kuwa Marefu

Niite nami nitakuitikia nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua… YEREMIAH 33:3 BIBLIA

Urefu wa maombi yetu hauleti tofauti yoyote kwa Mungu. Kile cha muhimu ni kwamba tuombe jinsi anavyotaka tuombe na kwamba maombi yetu yanaongozwa na Roho, ni ya kutoka moyoni, yenye wingi wa shukrani, na kuandamwa na imani. Kote katika Biblia, kuna maombi mafupi ya ajabu lakini yenye uwezo mwingi. Haya hapa baadhi yake::

  • Musa alimwombea dada yake: “Mpoze, Ee Mungu nakusihi sana.” (Hesabu 12:13).
  • Eliya aliomba: “Ee Bwana, Mungu wangu, nakusihi roho ya mtoto huyu imrudie ndani yake tena.” (1 Wafalme 17:21 BIBLIA).
  • Yesu aliomba: “Baba uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo” (Luka 23:34 BIBLIA).

Kuna nyakati ambazo utaomba maombi marefu kuliko nyakati zingine, lakini hakuna uhusiano kati ya dakika au masaa tunayoomba na iwapo Mungu anatusikiliza. Akiambiwa tu Neno moja kwa imani kutoka kwa moyo wa kweli linaweza kuufikia moyo wake na kuugusa mkono wake.


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwamba ninaweza kuomba kutoka kwa moyo wangu, bila kujali urefu au ufupi wa maombi yangu. Ninashukuru kuwa ninaweza kuwa tu mimi nikiwa nawe.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon