Maombi ya Kujikabidhi

Maombi ya Kujikabidhi

Umkabidhi Bwana njia yako, pia umtumaini, naye atafanya. —ZABURI 37:5

Tunapojaribiwa kuwa na wasiwasi au kujali kuhusu hali fulani katika maisha, tunaweza kuomba maombi ya “maombi ya kujikabidhi.” Mungu huingilia kati katika hali zetu tukimkabidhi.

Katika maisha yangu mwenyewe, niligundua kuwa kadri nilivyojaribu kushughulikia vitu mwenyewe, ndivyo maisha yangu yalivyozidi kuwa na mvurugiko mkubwa. Nilikuwa mtu wa kujitegemea na nikapata ikiwa vigumu kujinyenyekeza na kukubali kuwa nilihitaji usaidizi. Hata hivyo, nilipojikabidhi kwa Mungu katika maeneo hayo na kupata furaha ya kumtwika mizigo yangu yote, sikuamini kuwa nilikuwa nimeishi chini ya kiasi hicho kikubwa cha mshinikizo kwa muda mrefu hivyo.

Mkabidhi Bwana watoto wako, ndoa yako, mahusiano yako ya kibinafsi, na haswa kitu chochote unachojaribiwa kushughulikia. Ni Mungu peke yake kwa kweli anayejua linalohitajiwa kufanywa, na ni Yeye Pekee anayestahili kulifanya. Kadri tunavyojikabidhi kwa uaminifu, ndivyo tunavyomkaribia zaidi na kufurahia zaidi.

Aaminiye anayeweza kumtumainia Baba hata kama mambo yameharibika, ni, aaminiye aliyekomaa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon