Maombi ya Kweli Yatokayo Moyoni

Maombi ya Kweli Yatokayo Moyoni

Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. YAKOBO 5:16

Nasisitiza kuwa maombi ni kitu rahisi sana kuliko tunavyofikiria. Shukuru kwamba Mungu hajafanya maombi yatatize; ni rahisi kweli. Wakati mwingine watu hufanya maombi yawe makavu na magumu; wakati mwingine nia na “mifumo” yetu ya kidini hufanya maombi yasiweze kufikiwa na wengi wetu.

Ninakwambia ukweli nikisema kwamba Mungu anatamani maisha yetu ya maombi yawe ya kawaida na ya kufurahia. Anataka maombi yetu yawe ya kweli na ya kutoka moyoni, na anataka mawasiliano yetu naye yasiwe na vizuizi vya kanuni, kaida, masharti na ushikiliaji wa sheria. Anakusudia maombi kujumuishwa kama sehemu mojawapo ya maisha yetu ya kila siku—kitu rahisi tunachoweza kufanya kila siku.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwamba ninaweza kuongea nawe kama kawaida na kwa ukweli. Asante kwa kuwa ninaweza kuongea nawe kama rafiki, na ninaweza kujua kwamba wewe huwa hapo wakati wote ninaokuhitaji.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon