Maombi ya Sirini

Maombi ya Sirini

Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. —MATHAYO 6:6

Ingawa maombi mengine ni ya umma au vikundi, maisha yetu ya maombi ni ya maombi yanayofanywa katika mahali pa siri.

“Maombi ya sirini” yanamaanisha kwamba hatumwambii kila mtu tunayejua kuhusu tajriba zetu binafsi katika maombi na vile tunavyoomba. Tunaomba kuhusu masuala na watu ambao Mungu anaweka mioyoni mwetu, na tunaacha maombi yetu yawe kati yetu naye isipokuwa kama tuna sababu nzuri kweli ya kufanya vinginevyo. Tunakataa kufanya maombi yetu kuwa maonyesho ili kuwapendeza watu wengine.

Ili maombi yaitwe inavyofaa—“maombi ya sirini,” lazima yatoke katika moyo mnyenyekevu kama inavyodhihirika katika maombi ya mtoza ushuru aliyedharauliwa katika Luka 18: 10-14. Alinyenyekea, akainamisha kichwa, na kwa utulivu na unyenyekevu, alimwomba Mungu kumsamehe. Kama jibu la uaminifu wake, maisha yake yote ya dhambi yakafutwa kwa sekunde.

Mungu hajatupatia kifungu cha mwongozo wa maombi ambao ni tata na mgumu kufuata. Kuzungumza na Mungu ni njia rahisi yenye nguvu ya kumkaribia.


Jenga uhusiano wako na Mungu kwa kutumia muda naye kila siku.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon