Matarajio ya Furaha

Matarajio ya Furaha

Utanijulisha njia za uzima; mbele za uso wako ziko furaha tele; na katika mkono wako wa kuume mna mema ya milele. ZABURI 16:11

Furaha maishani ni kitu cha ajabu kuwa nacho. Huenda tukataka kuona mabadiliko katika hali zetu, lakini hatuna haja ya kuruhusu hali zisizopendeza kutufanya kuwa na dhiki. Tunaweza kushukuru kwamba furaha hufanya baadhi ya hizo hali zisizopendeza kuvumilika zaidi. Hata kama unapitia mambo magumu, unaweza kuwa na furaha katika maisha yako huku ukitarajia kitu kizuri kufanyika. Furaha inaweza kuwa tofauti kutegemea nguvu yake, kuna furaha ya utulivu na furaha ya kicheko. Inahusiana kwa karibu sana na matarajio yetu (kile tunachofikiri na kuamini). Maana mojawapo ya furaha ni: “Hisia au msisimko unaotokana na matarajio ya mema.” *Kwa maneno mengine, furaha yetu hutegemea matarajio yetu kuhusu vile vitu vitakavyofanyika katika maisha yetu. Usihofu au kutarajia mambo mabaya kukujia. Omba, amini, na utarajie mema ya Mungu kwa ajili ya maisha yako—halafu uone furaha yako ikiongezeka.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwa furaha yako. Leo nitaishi katika imani ya matarajio ya wema wako katika maisha yangu. Nitafurahia katika upendo na uaminifu wako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon