Mitihani ya Kweli Kabisa ya Tabia

Mitihani ya Kweli Kabisa ya Tabia

Na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini na tumaini halitahayarishi. —WARUMI 5:4

Tabia zetu hufunuliwa kwa usahihi kwa kile tunachofanya kwa siri. Ufunguo muhimu wa kuishi maisha yanayomkaribia Mungu katika uhusiano wa ndani naye, ni kuwa mtu mwenye tabia thabiti, kwa sababu unapogundua kwamba Mungu yuko nawe katika kila dakika ya kila siku- utaishi kumpendeza bila kujali iwapo mtu anakuona au la.

Watu wengi watafanya kitu kinachostahili wakati ule mtu anawatazama—kiongozi, mwajiri au mtu aliye na ushawishi—anatazama, lakini watafanya mambo kiholela wakati ule mtu hawatazami isipokuwa Mungu. Kama Wakristo, mchakato wa mawazo yetu unafaa kuwa, “Nitafanya kitu kinachostahili kwa sababu tu ninataka kumpendeza Bwana.”

Tabia pia huonekana tunapowatendea wengine mema hata kama kitu chema hakijaanza kufanyika kwetu bado. Yesu alituonyesha hili—Yeye “alipotukanwa, hakurudisha matukano, alipoteswa, hakuogofya” (1 Petro 2:23). Tunaweza kufuata mfano wa Yesu kwa kumtendea mema mtu asiyetutendea mema, kwa kumbariki mtu asiyetubariki, kwa kuwapenda watu wasiotupenda. Haya ndiyo mambo ambayo Yesu alitenda, na tukitaka kuwa kama yeye, tutahitaji kuchagua kuyafanya.


Tabia zetu huonekana katika jinsi tunavyochagua kutenda mema hata kama hatutaki kuyatenda.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon