Moyo Mchangamfu

Moyo Mchangamfu

Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; bali roho iliyopondeka huikausha mifupa. —MITHALI 17:22

Mungu ni uzima, na kila kitu kizuri alichoumba ni kimojawapo cha uzima huo. Tunaweza kushikika sana katika kufanya na kutimiza, katika kufanya kazi na kulipwa, kiasi kwamba tusipokuwa waangalifu, tutafikia hatima ya maisha yetu na kuamka ghafla na kugundua kwamba hatukuwahi kuishi kwa kweli. Mungu anatamani tufurahie maisha na tuyatimize, hadi yafurike.

Tuna uteuzi katika maisha. Tunaweza kunung’unika kuhusu shida zetu tunapopitia shida zetu, au tunaweza kumkaribia Mungu katika nyakati ngumu, tukipitia shida yoyote inayotukabili na moyo mchangamfu. Iweje, sisi sote tutakabiliana na shida kutoka wakati mmoja hadi mwingine, kwa hivyo kwa nini tusichukue furaha ya Bwana kama nguvu zetu na tujazwe na nguvu na uchangamfu?

Katika Yohana sura ya 15, Yesu anazungumza kuhusu kukaa ndani yake. Katika msitari wa 11 anasema, “Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.” Yesu alifanya ikawezekana sisi kuwa na mioyo michangamfu. Kwa uasidizi wake hata kama unapitia mambo gani, unaweza kutabasamu na kufurahia kila siku ya maisha yako ndani yake.


Usiishi kila siku ya maisha yako ukingoja vitu vibadilike kabla uwe na furaha. Fanya uamuzi wa kufurahi sasa hivi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon