Moyo wa Utiifu

Moyo wa Utiifu

Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake. —WARUMI 6:17

Paulo aliandika kwamba waaminio katika Roma walikuwa watiifu kwa mioyo yao yote. Hili lilikuwa muhimu kwa sababu inawezekana kuwa na utiifu nusu nusu—kuwa mtiifu kiulegevu katika tabia, lakini ukose kuwa mtiifu kifuraha kwa moyo wako wote.

Kutii kile Mungu amesema si jambo tu la kujionyesha, lakini jambo la kuwa na nia njema. Unapotaka kumpendeza Bwana kwa kweli, utataka kabisa kungoja mwelekeo na maagizo yake kwa maisha yako.

Ninataka kukuhimiza kuja juu zaidi katika utiifu wako. Usiwe aina ya mtu ambaye Mungu atalazimika kukabiliana naye kwa wiki nyingi ili tu akufanye ufanye hata kitu rahisi na kidogo sana. Fanya kwa furaha kile Mungu amekwambia ufanye.

Utiifu ni zaidi ya wajibu wa kiroho—ni nafasi ya kiroho! Utiifu wako kwa Mungu utatuzwa hatimaye. Utiifu hupanda mbegu inayohitajika kuleta baraka nyingine katika maisha yako. Huwezi kutoa zaidi ya Mungu; atatuza mbegu zako za utiifu kila mara.


Matokeo ya moyo mtiifu ni baraka za Mungu juu ya maisha yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon