Msingi wa Furaha

Hii ndiyo jumla ya maneno ; yote yamekwisha sikiwa; mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu (MHUBIRI 12:13)

Mwandishi wa Mhubiri alikuwa mwanamume ambaye alijaribu kufanya kila kitu ili awe na furaha. Alikuwa na mali nyingi, uwezo mkuu, na wake wengi. Hakujizuia raha yoyote ya dunia. Chochote ambacho jicho lake lilitamani alichukua. Alikula, kunywa na kufanya raha. Alikuwa na maarifa mengi, hekima, na heshima ilhali alichukia maisha. Kila kitu kikaanza kuonekana ubatili kwake. Akajaribu kutafuta maana ya maisha na akawa amechanganyikiwa zaidi na zaidi.

Mwishowe, alitambua chanzo cha shida yake. Hakuwa anatii amri za Mungu. Alikuwa hana furaha kwa sababu ya hilo na akatoa taarifa kwamba msingi wa furaha yote ni utiifu.

Kuna watu wengi wenye huzuni na kuomboleza wanaotembea wakilaumu watu wengine na hali kwa kukosa furaha bila kutambua kwamba sababu ya kutoridhika kwao ni kukosa kumtii Mungu.

Ninaamini unataka kuwa na furaha. Ufunguo wa furaha ni kumtii Mungu. Mhubiri 12:13 inasema kwamba utiifu ni kubadilisha hali zote zisizokubaliana  na utaratibu wa Mungu. Hiyo ina maana kwamba chochote kilicho nje ya utaratibu au mpangilio kilikuja kuwa hivyo kupitia kwa ukaidi, na utiifu ndio unaoweza kuleta utaratibu. Kila wakati tunapomtii Mungu, kuna kitu katika maisha yetu ambacho huboreka.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Jizatiti kumtii Mungu katika mambo yote na furaha yako itazidi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon