Mungu Ana Mpango

Mungu ana Mpango

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. —YEREMIA 29:11

Iwapo una picha mbaya binafsi kujihusu, tayari imeathiri vibaya mambo yake ya kale, lakini unaweza kuponywa na kutoruhusu ya kale kujirudia. Ninakuhimiza kusahau yaliyopita hata mambo yoyote hasi ambayo umehisi kujihusu na kujisukuma mbele kuelekea vitu ambavyo Mungu amekuwekea.

Mungu ana mpango mwema na kusudi kwa kila mmoja wetu na njia maalum na wakati mtimilifu wa kuyafanya yatimie, lakini sio sisi wote tunayaona haya. Wakati mwingi tunaishi chini ya kiwango cha maisha ambayo Mungu anakusudia tufurahie.

Kwa miaka mingi sikutumia haki na faida zangu kama mwana wa Mungu. Ingawa nilikuwa Mkristo na kuamini nitaenda mbinguni nitakapofariki, sikujua kwamba kuna jambo ambalo lingefanywa kuhusu maisha yangu yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Nilikuwa na picha mbaya kujihusu, na ikaathiri maisha yangu ya kila siku, pamoja na mwono wangu wa siku zijazo.

Leo unaweza kukubali upendo wa Mungu juu yako na uufanye upendo wake msingi wa kujipenda na kujikubali. Pokea hakikisho lake, ukijua kwamba unabadilika na kuwa vile anavyotamani uwe. Halafu uanze kujifurahisha—ulipo—ukiwa njiani kuelekea ukomavu mkamilifu wa kiroho.


Acha Mungu awe Mungu katika maisha yako. Mweke katika kiti cha dereva. Anajua analofanya.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon