Mungu Anaweza

Mungu Anaweza

Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu. —WAEFESO 3:20

Waefeso 3:20 ni andiko lenye nguvu ambalo linatuambia kuwa Mungu wetu anaweza—anaweza kufanya mambo ya ajabu mno kuliko tuyaombayo, kutumainia au hata kuwaza. Tunaweza kuomba, na kuomba kwa imani na matumaini. Lakini ni Mungu anayefanya kazi, sio sisi. Anaifanya vipi? Kulingana na nguvu au neema ya Mungu ifanyayo kazi ndani yetu. Chochote tunachopokea kutoka kwa Mungu kinahusiana moja kwa moja na kiasi cha neema tunayojifunza kupokea.

Nilikuwa nikijiwekea mfadhaiko mkuu nikijaribu kubadilika. Nilikuwa chini ya hukumu kuu kwa sababu kila ujumbe niliokuwa nikisikia ulionekana kuniambia nibadilike; ilhali nisingebadilika hata ningejaribu vipi. Nilikuwa katika mateso makuu kwa sababu niliona vitu vyote kunihusu ambavyo vilihitaji kubadilishwa, lakini sikuwa na uwezo wa kufanya mabadiliko hayo.

Kadri unavyosonga karibu na Bwana, ndivyo unavyoona kwamba lazima awe Chanzo chako katika vitu vyote. Ni yeye pekee anayeweza kuleta mabadiliko katika maisha yako. Jifunze kusema, “Mungu, siwezi kufanya chochote bila Wewe, lakini unaweza kufanya mambo yote kupitia kwangu!”


Mungu anaahidi kututia nguvu katika udhaifu wetu tukimwamini na kumgeukia. Neema ya Mungu itatosha kukutana na mahitaji yetu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon