Mungu Huchagua Karama Zetu

Hawezi mtu kupokea neno lolote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni (YOHANA 3:27) 

Ninafikiri kitu cha huzuni hufanyika watu wanaposhindana au kujilinganisha na wengine katika eneo la karama za kiroho, uwezo wa kawaida, na miito ambayo Mungu ameweka juu ya maisha yao. Mlinganisho na mashindano hutufanya tupoteze furaha ya kuwa na kufanya kile ambacho Mungu ametupangia kuwa na kufanya.

Andiko la leo linatuagiza kuridhika na karama au karama tulizo nazo. Karama zetu hutoka kwa Mungu na tunahitaji kufurahia karama anazotupa kwa sababu hatutapata karama zingine zozote hadi Mungu aamue kutupatia. Tunahitaji kumwamini Roho Mtakatifu, tukiamini kwamba ametumwa duniani kusaidia kuhakikisha kwamba mapenzi ya Mungu yanatimia duniani na maisha ya kila mmoja wetu.

Ninakuhimiza kutafakari juu ya ukweli kwamba Mungu amemtuma Roho Mtakatifu kuishi ndani yetu. Kwa kweli anaishi ndani ya kila mtu ambaye kwa kweli amemkubali Yesu Kristo kama Mwokozi na Bwana. Roho Mtakatifu alitumwa kutuhifadhi hadi siku ya mwisho ya wokovu atakaporudi Yesu kudai wana wake. Anajaribu kuzungumza nasi ili akatuongoze katika ukamilisho wa kile ambacho Yesu alikufa ili tuwe nacho. Tunapopinga mwito wetu au kutoridhika na jinsi tulivyo na tulicho nacho, tunapinga kazi na hekima ya Roho Mtakatifu. Tunahitaji kujisalimisha kwake, kutii sauti yake, kukuza karama alizoweka ndani yetu, na kwa usaidizi wake, tuishi maisha yetu kwa shauku na ukamilisho kwa utukufu wa Mungu.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO: Ridhaa ni sifa kwa Mungu. Inamwambia kwamba tunamwamini na kufurahia yote anayotutendea.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon