Mungu Hutuongoza kwa Kutumia Amani

Mungu Hutuongoza kwa Kutumia Amani

Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote. 2 WATHESALONIKE 3:16

Mara nyingi watu hufanya vitu wasivyokuwa na amani kuvihusu, kisha wanashangaa ni kwa nini wana fujo nyingi katika maisha yao. Tukifuata Neno la Mungu na kushukuru kwa ajili ya uelekezi na uongozi wake, tutafurahia maisha ya baraka na amani. Biblia inatuonya kwamba tutaishi katika laana tukifuata mapenzi yetu wenyewe na kutembea katika njia zetu (tazama Kumbukumbu la Torati 28:15–33).

Mara nyingi husikia watu wakisema vitu kama vifuatavyo:
• “Ninajua sifai kufanya hiki lakini . . .”
• “Ninajua sifai kununua hiki lakini . . .”
• “Bila shaka sifai kusema hiki lakini . . .”

Maneno haya yanaakisi hisia inayofadhaisha ndani kabisa, “kujua” kwamba kitendo wanachofanya si kizuri au kizuri kwao, lakini wanakataa kusalimisha hiari zao kwa uongozi wa Mungu.
Shukuru kwamba, tunapohisi kukosa amani, tunaweza kuamua kuachilia mipango yetu na kujisalimisha kwa mpango mzuri wa Mungu juu ya maisha yetu.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwamba unaniongoza kwa kutumia amani. Nisaidie kutambua uongozi wa Roho wako unapoimarisha mwelekeo wa maisha yangu. Asante kwa amani inayokuja kwa kujua kwamba uko mamlakani na una mpango mwema kwa ajili yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon