Ni Maoni ya Nani yaliyo Sahihi?

Ni Maoni ya Nani yaliyo Sahihi?

Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu, halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolitumia. ISAYA 55:11

Maoni yanafurahisha sana kwa kuwa sisi wote tunayo maoni tofauti. Una haki ya kuwa na maoni yako, lakini hilo halina maana kuwa uwe ukiwapa wenzako wakati wote. Mara nyingi watu hukataa maoni yetu; na hata wakituomba tuwaambie, huwa wanatumai kuwa tutakubaliana na maoni waliyo nayo tayari. Hekima hujua wakati wa kuongea na wakati wa kunyamaza.

Tunafaa kuwa na hekima kuhusu vile tunavyotoa maoni yetu kwa uhuru, na tunafaa pia kupinga kukubali maoni ya watu wengi kwa sababu ni ya watu wengi. Shukuru kuwa Mungu ametupatia ukweli wake ambao unaweza kuumba na kuunda maoni yetu. Iwapo tutaamua kuwa Neno la Mungu lisilobadilika ndilo litakuwa msingi wa fikra na maoni yetu, bila kujali vile utamaduni unavyosema au maoni ya wengi wakati huo; Mungu atakutuza kwa sababu Neno lake halimrudii bure.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwa Neno la heri la Mungu ambalo hunipa ukweli ninaojenga fikra, nia na maoni yangu juu yake. Nisaidie kujua tofauti kati ya kitu kinachopendwa na wengi wakati huo na kile cha kweli kisichobadilika. Nisaidie kuunda maoni ya hekima na yenye kuhimiza.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon