Ni Sawa Kuwa Tofauti

Ni Sawa Kuwa Tofauti

Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota. 1 WAKORINTHO 15:41

Sisi wote ni tofauti. Kama jua, mwezi, na nyota, Mungu ametuumba kuwa tofauti na kila mmoja, na amefanya hivyo maksudi. Kila mmoja wetu hutimiza hitaji, na sisi wote ni sehemu mojawapo ya mpango jumla wa Mungu.

Kwa shukrani, tunaweza kuwa watu salama, tukijua kuwa Mungu anatupenda na ana mpango juu ya maisha yetu. Hatupaswi kutishiwa na uwezo wa watu wengine. Tunaweza kuwa huru kupenda na kujikubali pamoja na kuwakubali wengine bila kuhisi mshinikizo wa kujilinganisha au kushindana.

Tuking’ang’ana kuwa kama watu wengine, hatutajisahau tu lakini tunamhuzunisha Roho Mtakatifu. Mungu anatutaka tutoshee katika mpango wake; hataki tuhisi mshinikizo wa kutoshea katika mpango wa kila mtu. Tofauti ni sawa; ni sawa kuwa tofauti.


Sala ya Shukrani

Baba, umeniumba niwe tofauti na wa kipekee, na ninakushukuru kwa sababu ya hilo. Kwa usaidizi wako, nitaepuka hayo majaribu ya kujilinganisha na watu wengine. Nitapata usalama katika vile ulivyoniumba kuwa leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon