Nia Chanya

Nia Chanya

Mtu wa nia mbili husitasita katika njia zake zote. — YAKOBO 1:8

Tukipeleka matakwa yetu kwa Mungu katika maombi halafu tuendelee kuwa na wasiwasi kuyahusu, kwa kweli tutakuwa tunapinga imani yetu. Maombi ni nguvu chanya, na wasiwasi ni nguvu hasi. Tukizijumlisha pamoja tunapata sufuri. Sijui kukuhusu, lakini sitaki kuwa na uweza sufuri, kwa hivyo kwa usaidizi wa Mungu ninajaribu kutochanganya maombi na wasiwasi

Hata ingawa tunataka kuishi maisha yenye mafanikio na uweza mwingi, watu wengi hufanya mambo kwa uweza sufuri kwa sababu huwa wanachanganya yaliyo chanya na yaliyo hasi. Wanakiri vizuri kwa muda mfupi, kisha kukiri vibaya kwa muda mfupi. Wanaomba kwa muda mfupi kisha wanakuwa na wasiwasi kwa muda mfupi. Wanaamini kwa muda mfupi, kisha wanashuku kwa muda mfupi. Matokeo ni kwamba wanarudi nyuma na mbele bila kupiga hatua yoyote.

Hebu tusiyafanye mabaya kuwa makubwa—acha tuyafanye mazuri kuwa makubwa! Acha tuinue mambo mazuri ambayo Yesu anafanya kwa kuzungumza kuyahusu, kwa mawazo mazuri, katika mielekeo yetu, jinsi tunavyokaa, katika maneno yetu na katika matendo yetu.
Kwa nini usifanye uamuzi wa kutarajia mema kwa kumwamini Mungu na kukataa kuwa na wasiwasi?


Jizoeshe kuwa na fikra nzuri katika kila hali inayotokea. Hata kama kile kinafanyika wakati huo si kizuri sana, tarajia Mungu kuleta wema kutokana nacho.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon