Kujikubali Ulivyo Ukiwa Njiani Kuelekea Unakoenda

Usiogope maana hutatahayarika wala usifadhaike maana hutaaibishwa kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena. — ISAYA 54:4

Ni muhimu kujikubali na kujikumbatia. Jiulize iwapo unajipenda. Iwapo hujipendi, utakuwa na wakati mgumu kumpenda mtu mwingine yeyote. Iwapo hujipendi utakuwa na matatizo na wengine.

Tunapokuwa katika uhusiano wa karibu na Bwana, tunaweza kutulia tukijua kwamba kukubaliwa kwetu hakutegemei mambo tunayofanya au tabia timilifu, lakini kwa kazi ambayo Yesu ametufanyia na kufanya ndani yetu. Kukubaliwa kwetu kunategemea uhusiano wetu binafsi na Yesu.

Kujipenda kunamaanisha tujikubali kama viumbe wa Mungu. Hatuhitaji kupenda kila kitu tunachofanya ili kujipenda na kujikubali. Mungu anatupenda bila masharti, na hata kama tunafanya makosa hatupunguzi kuwa wanawe.

Ninakuhimiza kujitazama kwenye kioo kila asubuhi na kusema, “Ninajipenda. Mimi ni mwana wa Mungu na ananipenda. Nina vipawa na talanta. Mimi ni mtu wa kipekee—na ninajipenda na kujikubali.” Ukifanya hivyo na kwa kweli uamini, itafanya maajabu katika kukusaidia kukubali mtu ambaye Mungu alikuumba uwe.


Unaweza kuwa na amani kuhusu maisha yako yaliyopita, uridhike na yaliyopo, na kuwa na hakikisho la siku zako zijazo, ukijua yako katika mikono ya upendo ya Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon